Paco Jemez-Ni fedheha kupigwa bao 10-2

Haki miliki ya picha AP

Bosi wa Timu Rayo Vallecano Paco Jemez amesema Timu yake ilifedheheshwa na kudhalilishwa ilipobamizwa Mabao 10-2 wiki hii kwenye Mechi ya La Liga Uwanjani Santiago Bernabeu.

Amesema kipigo hicho kimeaibisha Soka la Spain na kuipotezea imani.Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Real Madrid kufunga Bao 10 kwenye Mechi ya La Liga tangu Mwaka 1960 walipoifunga Elche 11-2.

Akijibu madai ya Jimenez, Kocha wa Real, Rafa Benitez, alisema: "Kuna mechi nyingi hata sisi tulionewa, hatukunufaika. Sikusema lolote wakati huo na sitasema kitu sasa.”

Ligi kuu ya Hispania kwa sasa inaenda Mapumziko ya Siku 10 kwa ajili ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya.