Mabondia kuzipiga Krismasi Tanzania

Mabondia wa Tanzania Francis Cheka na Thomas Mashali (simba asiyefugika), leo watakuwa wakipigana katika pambano lisilo la ubingwa litakalofanyika katika uwanja wa jamhuri mjini Morogoro pambano ambalo ni burudani kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Krismasi.

Mabondia hao wenye uzito wa juu tayari wameshapima uzito Kkuelekea katika pambano hilo ambapo mabondia wote wawili wameendelea kutambiana huku wakiwataka mashabiki kujitokeza kushuhudia pambano hilo lililoandaliwa na promota mkubwa wa Tanzania Kaike Siraji kupitia (Kaike promosheni).