Miamba kuwa mawindoni EPL

City Haki miliki ya picha Getty
Image caption Manchester City watakutana na Sunderland

Ligi kuu ya soka ya England itaendelea Jumamosi siku ya Boxing Dei kwa michezo kumi Man City na Chelsea wakiwa mawindoni nyumbani, Man Utd na Arsenal nao wakiwa ugenini.

Stoke City ndio watakaokuwa wenyeji wa Manchester United, Aston Villa wawe wenyeji wa West Ham, huku Bournemouth wakiwaalika Crystal Palace.

Chelsea watakuwa nyumbani dhidi ya Watford, Liverpool watakuwa nyumbani Anfield dhidi ya viongozi wa ligi Leicester city, Man City watawakaribisha Sunderland, nao Southampton watakuwa wenyeji wa Arsenal.

Na Idhaaa ya kiswahili ya BBC itakutangazia mchezo kati ya Manchester City na Sunderland kupitia matangazo yake ya Ulimwengu wa soka.

Ratiba kamili ya mechi za Jumamosi 26 Desemba (Saa za Afrika Mashariki)

 • Stoke v Man Utd 15:45
 • Aston Villa v West Ham 18:00
 • Bournemouth v Crystal Palace 18:00
 • Chelsea v Watford 18:00
 • Liverpool v Leicester 18:00
 • Man City v Sunderland 18:00
 • Swansea v West Brom 18:00
 • Tottenham v Norwich 18:00
 • Newcastle v Everton 20:30
 • Southampton v Arsenal 22:45

Mechi za Jumatatu 28 Desemba

 • Crystal Palace v Swansea 18:00
 • Everton v Stoke 18:00
 • Norwich v Aston Villa 18:00
 • Watford v Tottenham 18:00
 • West Brom v Newcastle 18:00
 • Arsenal v Bournemouth 20:30
 • Man Utd v Chelsea 20:30
 • West Ham v Southampton 20:30

Jumanne 29 Desemba 2015

 • Leicester v Man City 22:45

Jumatano 30 Desemba 2015

 • Sunderland v Liverpool 22:45