Arsenal wamtafuta nyota wa Basel

Elneny Haki miliki ya picha Getty
Image caption Elneny huchezea timu ya taifa ya Misri

Arsenal wameanzisha mazungumzo na klabu ya FC Basel wakitaka kumchukua kiungo wa kati Mohamed Elneny.

Mchezaji huyo wa umri wa miaka 23 huchezea timu ya taifa ya Misri na alijiunga na klabu hiyo ya Uswizi mwaka 2013.

Ameshinda taji la ligi na klabu hiyo misimu mitatu ambayo amekuwa nchini humo.

Bei yake inakadiriwa kuwa karibu £5 milioni ingawa atahitaji kibali cha kufanyia kazi Uingereza.

Anaweza kuwachezea Arsenal Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwani Basel hawakuweza kufuzu kwa hatua ya makundi mwaka huu.

Elneny alichezea Basel mechi ya nyumbani ambayo walifanikiwa kulaza Chelsea msimu wa 2013-14.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anajaribu kutia nguvu safu yake ya kati baada ya Francis Coquelin na Santi Cazorla kupata majeraha mabaya ya magoti. Aaron Ramsey na Mikel Arteta pia wamekosa michezo kadha kutokana na majeraha.

Hata hivyo, Elneny anatazamwa na Wenger kama mchezaji wa kufaa Gunners kwa muda mrefu bali na kusaidia kujaza pengo la sasa.