Azam yashinda, Toto yachapwa

Image caption Azam FC

Ligi kuu ya Tanzania bara jana iliendelea tena kwa michezo miwili kuchezwa.

Azam Fc, wakicheza katika uwanja wao wa Azam Complex, walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Mabao ya Azam yakifungwa na Kipre Tchetche na Shomari Kapombe, huku Salum Kanoni wa Kagera akikosa mkwaju wa penati baada ya kipa wa Azam Aishi Manula kuupangua.

Na katika dimba la CCM Kirumba mjini Mwanza wenyeji Toto Afrikans walichapwa kwa bao 1-0 dhidi ya Afrikan Sport ya Tanga.

Ligi hiyo itaendelea tena kutimua vumbi Decemba 30 mwaka huu.