Uingereza yashinda Afrika Kusini kriketi

Kriketi Haki miliki ya picha AP
Image caption Huu ni ushindi wa pili wa Uingereza ugenini tangu 2012

Uingereza imepata ushindi wa wiketi sita kwa mikimbio 38 pekee siku ya tano ya mechi ya kimataifa na kukamilisha ushindi wa mikimbio 241 dhidi ya Afrika Kusini mjini Durban.

Afrika Kusini walirejea uwanjani wakiwa 136-4 wakitafuta kufikia 416 lakini wakashindwa wiketi nne kwa mikimbio saba katika ova tisa.

Moeen Ali alimuondoa AB de Villiers kwa mpira wa tatu naye Steven Finn akamaliza na 4-42.

Mechi ya pili ya shindano la sasa la mechi nne itachezwa mjini Cape Town Jumamosi.

Ushindi wa leo umekuwa wa pili katika mechi ya kimataifa ugenini tangu 2012 na ndio wao mkubwa zaidi kwa mikimbio dhidi ya Afrika Kusini tangu 1991.

Afrika Kusini, maarufu kama Proteas sasa wameenda mechi saba bila kushinda, ambacho ndicho kipindi kirefu zaidi kwenda bila ushindi tangu warejeshwe kriketi ya kimataifa 1991.