Liverpool yaichapa Sunderland

Haki miliki ya picha PA

Majogoo wa Anfield Liverpool wakiwa ugenini katika dimba la light wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Sunderland.

Mshambuliaji Christian Benteke ndie aliyefunga bao hilo pekee lililoipa timu yake ushindi na pointi tatu muhimu.

Kwa ushindi huo klabu ya Liverpool imejikita katika nafasi ya 7 kwa alama 30 baada ya kuwa imecheza michezo 19 msimu huu.

Sunderland maarufu kama paka weusi wanasalika katika nafasi ya 19 wakiwa na alama 12 baada ya kucheza michezo 19.