Leicester City wahangaisha Man City

Kipa Haki miliki ya picha Getty
Image caption Golikipa Kasper Schmeichel alichangia sana kuzuia Manchester City kufunga

Klabu ya Leicester City imeendelea kushangaza katika Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kutoka sare tasa na miamba Manchester City Jumanne.

Kutokana na sare hiyo, Leicester sasa wana alama sawa na viongozi wa ligi Arsenal, ingawa wako nambari mbili ukizingatia tofauti ya mabao.

Man City ndio waliotawala mchezo huo uliochezewa dimba la King Power kwa asilimia 61, huku wenyeji Leicester wakimiliki kwa asilimia 39 .

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Leicester imeshangaza wengi kwa kuendelea kukwamilia nafasi za juu ligini

Wachezaji wa Man City Aleksandar Kolarov, Kevin De Bruyne, Eliaquim Mangala walipewa kadi za manjano huku Marc Albrighton wa Leicester naye akipewa kati ya njano na mwamuzi Craig Pawson.

Ligi hiyo itaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa Paka Weusi wa Sunderland watawaalika majogoo wa jiji la Anfield katika dimba la Stadium of Light.

Jedwali la EPL lilivyo kwa sasa:

Nambari Klabu Mechi Mabao Alama
1 Arsenal 19 15 39
2 Leicester 19 12 39
3 Man City 19 17 36
4 Tottenham 19 18 35
5 Crystal Palace 19 7 31
6 Man Utd 19 6 30
7 West Ham 19 5 29
8 Watford 19 4 29
9 Stoke 19 1 29
10 Liverpool 18 -1 27
11 Everton 19 7 26
12 Southampton 19 3 24
13 West Brom 19 -6 23
14 Chelsea 19 -6 20
15 Norwich 19 -10 20
16 Bournemouth 19 -12 20
17 Swansea 19 -8 19
18 Newcastle 19 -15 17
19 Sunderland 18 -18 12
20 Aston Villa 19 -19 8