Srnicek afariki duniani

Image caption Uwanja wa mpira wa timu ya Newcastle

Golikipa wa zamani wa Newcastle Pavel Srnicek amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 47.

Umauti umemfika golikipa huyu baada ya kusumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa moyo uliomsumbua kwa muda wa siku nane.

Srnicek, enzi za uhai wake alivichezea vilabu ya Sheffield Wednesday, Portsmouth na West Ham, huku akidakika timu yake ya taifa ya Jamuhuri ya Czech, michezo 49.

Mlinda mlango huyu aliidakia Newcastle jumla ya michezo 190 kuanzia miaka ya 1990 mpaka 2007.