MOJA KWA MOJA: Mechi za EPL Jumamosi

Bofya hapa kwa habari za karibuni zaidi

19:56 MECHI ZINAMALIZIKA

 • West Ham 2-0 Liverpool
 • Arsenal 1 -0 Newcastle
 • Leicester 0-0 Bournemouth
 • Man Utd 2-1 Swansea
 • Norwich 1 -0 Southampton
 • Sunderland 3-1 Aston Villa
 • West Brom 2-1 Stoke

19:53 Manchester United 2-1 Swansea

David de Gea anafanya kazi ya ziada kumzuia Ashley Williams kufunga.

19:51 Sunderland 3-1 Aston Villa

Jermain Defoe anafungia Sunderland bao la tatu.

19:50 West Brom 2-1 Stoke

Jonny Evans anafungia West Brom bao, ambao huenda likawahakikishia ushindi. Ni dakika ya 93. Hilo ndilo bao lake la kwanza tangu 2012.

19:48 Arsenal 1-0 Newcastle

Sekunde chache baadaye, Mesut Ozil anatikisa wavu, lakini kutoka upande wa nje.

19:47 Arsenal 1-0 Newcastle

Aaron Ramsey anapoteza nafasi nzuri ya kufunga. Mpira wake unatoka nje.

19:45 West Brom 1-1 Stoke

Geoff Cameron wa Stoke anaonyeshwa kadi nyekundu.

19:38 Baooo! West Brom 1-1 Stoke

Huko Hawthorns, Jon Walters anasawazishia Stoke City.

19:35 Baooooo! Manchester United 2-1 Swansea

Wayne Rooney anafungia Man Utd la pili dakika ya 75 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Anthony Martial .

19:33 Baoooo! Norwich 1-0 Southampton

Alexander Tettey anafungia Norwich dakika ya 74.

19:32 Sunderland 2-1 Aston Villa

Jermain Defoe anarejesha Sunderland mbele.

19:30 Norwich 0-0 Southampton

Mkenya Victor Wanyama anapewa kadi nyekundu.

19:29 Baooo!Arsenal 1-0 Newcastle

Laurent Koscielny anaweka Arsenal kifua mbele.

19:29 Baooooo! Manchester United 1-1 Swansea

Gylfi Sigurdsson anasawazishia Swansea.

19:22 Manchester United 0-0 Swansea

Andre Ayew anapata nafasi. Anajipenyeza kati ya walinzi wawili wa Man Utd lakini mpira wake wa kichwa unagonga mlingoti wa goli.

19:20 Baoooo! Sunderland 1-1 Aston Villa

Carles Gil anasawazishia Aston Villa.

19:17 Baooo!West Brom 1-0 Norwich

Stephane Sessegnon anafungia West Brom.

19:15 Leicester 0-0 Bournemouth

Riyad Mahrez anashindwa kufunga penalti.

19:14 Leicester 0-0 Bournemouth

Leicester wanapata penalti na Simon Francis wa Bournemouth anaonyeshwa kadi nyekundu kwa kumwangusha Jamie Vardy.

19:09 Leicester 0-0 Bournemouth

Leicester wanapoteza nafasi nzuri sana ya kufunga.

Jamie Vardy anatoa kombora lakini linatemwa nje. Kona inapigwa lakini mpira wa Wes Morgan unapaa juu ya wavu.

19:07 BAOOO! Manchester United 1-0 Swansea

Anthony Martial anafungia Man Utd kwa kichwa.

Haki miliki ya picha Reuters

19:04 Manchester United 0-0 Swansea

Phil Jones ameumia na badala yake anaingia Matteo Darmian.

19:01 Leicester 0-0 Bournemouth

Leicester wanaingiza Nathan Dyer nafasi ya Leo Ulloa.

19:01 KIPINDI CHA PILI

18:45 WAKATI WA MAPUMZIKO

 • Arsenal 0-0 Newcastle
 • Leicester 0-0 Bournemouth
 • Man Utd 0-0 Swansea
 • Norwich 0-0 Southampton
 • Sunderland 1-0 Aston Villa
 • West Brom 0-0 Stoke

18:44 Manchester United 0-0 Swansea

Juan Mata anashambulia tena, lakini mpira wake unatua mikononi mwa kipa Lukasz Fabianski.

18:39 Manchester United 0-0 Swansea

Mpira mzuri kutoka kwa Ashley Young kulia unaelekezwa eneo la hatari na nahodha Rooney anaruka juu kuufikia kwa kichwa, lakini Angel Rangel wa Swansea anampiku na kuuelekeza salama kwa kipa Lukasz Fabianski.

18:38 Arsenal 0-0 Newcastle

Mesut Ozil anashambulia lakini juhudi zake zinazimwa na Jack Colback anayemwangusha.

Haki miliki ya picha PA

18:37 Manchester United 0-0 Swansea

Man United wanashambulia. Juan Mata anapiga mpira wa adhabu upesi sana baada ya Anthony Martial kuangushwa nje tu ya eneo la hatari. Mata analenga goli lakini mpira unaenda moja kwa moja hadi kwa kipa Lukasz Fabianski.

18:34 Manchester United 0-0 Swansea

Old Trafford, Man Utd hawajafanikiwa kufanya shambulio lolote hatari.

18:30 BAOOOO! Sunderland 1-0 Aston Villa

Mchezaji wa zamani wa Chelsea Patrick van Aanholt anafungia Sunderand bao la kwanza.

18:17 Arsenal 0-0 Newcastle

Newcastle wanafanya shambulio nadra na kumfanyisha kazi ya ziada kipa wa Arsenal Petr Cech, baada ya Georginio Wijnaldum kutuma mpira wa kichwa. Baada ya Cech kuutema, Jack Colback anaurejesha tena lakini Arsenal wananusurika.

18:12 Uwanjani King Power, Riyad Mahrez wa Leicester anatoa kombora lakini anazidisha nguvu na mpira wake unapaa juu ya wavu unaolindwa na Bournemouth.

18:10 Katika mechi ya klabu zilizo chini kwenye jedwali, wenyeji Sunderland wanaokolewa na Vito Mannone baada ya mpira kutoka kwa Jordan Veretout aliyepewa pasi na Leandro Bacuna.

18:03 Arsenal wanaanza kwa kushambulia. Alex Oxlade-Chamberlain anapata nafasi lakini anashindwa kudhibiti kombora lake.

18:00 Mechi zinaanza.

17:55 Mechi zinazoanza saa kumi na mbili unusu saa za Afrika Mashariki ni zifuatazo:

 • Arsenal v Newcastle 18:00
 • Leicester v Bournemouth 18:00
 • Man Utd v Swansea 18:00
 • Norwich v Southampton 18:00
 • Sunderland v Aston Villa 18:00
 • West Brom v Stoke 18:00

Jedwali la msimamo wa ligi ya EPL

17:50 Hujambo? Karibu kwa habari za moja kwa moja kuhusu mechi za ligi ya EPL.

Klabu nyingi Uingereza zimeshuka dimbani kusaka alama za kwanza Mwaka Mpya, Arsenal wakijaribu kuendeleza uongozi kileleni.

Tayari mechi ya kwanza ya mapema imemalizika, Liverpool wakilazwa 2-0 na West Ham ugenini.

Miamba wengine watanusurika?

Arsenal watajaribu kuimarisha nafasi yao kileleni dhidi ya Newcastle, Manchester United nao wakijaribu kumaliza mkosi dhidi ya Swansea.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsenal wanaongoza ligi