Kyrgios amchapa Alexander katika tenisi

Haki miliki ya picha Reuters

Nyota wa mchezo wa tenesi wa Austalia Nick Kyrgios jana aliibuka na ushindi dhidi ya Mjerumani Alexander Zverev.

Kyrgios alianza kwa kupoteza seti ya kwanza kisha akashinda kwa seti 6-4 6-1 6-4 katika mchezo uliochukua muda wa saa moja.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anakabiliwa na mchezo dhidi ya bingwa namba mbili duniani Andy Murray katika mchezo wa Jumatano wa Hopman Cup. Murray kwa sasa yupo chini ya kocha mama yake Judy Murray.