Benitez: Ilikuwa heshima kubwa Real Madrid

Real Haki miliki ya picha Getty
Image caption Benitez aliongoza Real Madrid miezi saba

Rafael Benitez amesema ilikuwa ‘heshima kubwa’ kuwa mkufunzi mkuu wa Real Madrid, siku moja baada yake kufutwa kazi klabu hiyo ya La Liga.

“Kama Mwanamadrid kutoka Madrid, anayeelewa utamaduni na maadili ya klabu hii, imekuwa heshima kubwa kufanyia kazi rangi hizi za klabu hii,” amesema kupitia taaifa.

Ameongeza: “Ningependa kushukuru kila mmoja ambaye tangu siku ya kwanza aliniunga mkono na kufanya kazi yangu kuwa rahisi.’

Mhispania Benitez, mwenye umri wa miaka 55, aliachishwa majukumu yake baada ya mkutano wa bodi ya klabu hiyo siku ya Jumatatu.

Nafasi yake ilipewa mkufunzi mkuu wa timu B, mchezaji wa zamani wa Ufaransa Zinedine Zidane.

Benitez alipoteza mechi tatu kati ya michezo 25 na kuwaongoza Real kufika hatua ya 16 katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Rekodi ya Rafa Benitez

Real Madrid wamemfuta kazi

3

Nafasi ya Real kwa sasa La Liga

  • 4 Alama walizo nyuma ya viongozi Atletico Madrid

  • 7 miezi aliyohudumu mkataba wake wa miaka 3

  • 1 Mchezaji asiyefaa(Denis Cheryshev) aliyechezeshwa Copa del Rey - na kufanya Real Madrid kuondolewa michuano hiyo

Getty

Katika taarifa yake, Benitez amemuunga mkono Zidane na wachezaji wa timu hiyo.

"Baada ya kusema hayo yote, ningependa kumtakia kila la kheri Zinedine Zidane, mrithi wangu, na wasaidizi wake. Kwa wachezaji, wakufunzi na wafanyakazi, nawatakia kila la kheri.”