Sudan kuwa mwenyeji wa Cecafa 2016

Uganda Haki miliki ya picha FUFA
Image caption Uganda walishinda Kombe la Cecafa 2015 kwa kulaza Rwanda kwenye fainali

Sudan ndiyo itakayokuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Cecafa mwaka huu, Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati limetangaza.

Taifa hilo liliandaa michuano hiyo mara ya mwisho 2013.

Uganda ndiyo itakayokuwa mwenyeji wa michuano ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 yaani Cecafa Under-17 na pia michuano ya ubingwa upande wa wanawake mwaka huu.

Burundi itakuwa mwenyeji wa fainali za wachezaji wa chini ya miaka 20.

Cecafa pia imetangaza mpango wa miaka mitano ambao uutasisitiza ukuaji wa soka ya chipukizi na wanawake pamoja na kuimarisha uwezo wa kiufundi.

Hayo yakijiri, rais wa Shirikisho la Soka la Somalia Abdiqani Said Arab ameteuliwa naibu mwenyekiti wa Cecafa.