Manchester City hoi Capital One

Haki miliki ya picha AFP

Klabu ya soka ya Everton imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester City katika michuano ya Kombe la Ligi nchini Uingereza.

Wachezaji Funes Mori na Romelu Lukaku ndio waliokuwa mashujaa katika uwanja wa Goodson Park kwa kuifungia klabu hiyo kwenye mechi hiyo ya kwanza ya nusu fainali kati ya klabu hizo mbili.

Mechi za marudiano zitachezwa kati ya Januari 26 na 27, ambapo kutoka kwa nusu fainali hiyo nyingine Livrpool watakuwa wenyeji wa Stoke City katika uwanja wa Anfield nao Man City watawakaribisha Everton katika dimba la Etihad.

Liverpool walilaza Stoke 1-0 mechi iliyochezwa Jumanne usiku.