Bale aifungia Real Madrid 'hat-trick'

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Gareth Bale

Mchezaji Gareth Bale alifunga mabao matatu na kumfanya kocha mpya wa kilabu ya Real Madrid Zinedine Zidane kupata ushindi wa kwanza katika kazi yake dhidi ya Deportivo La Coruna.

Karim Benzema alifunga bao lake la 100 katika ligi ya Uhispania alipoiweka timu yake kifua mbele katika dakika za kwanza tangu kuondoka kwa aliyekuwa mkufunzi Rafael Benitez.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Zinedine Zidane

Bale alifunga bao la pili ,la tatu na la nne na hivyobasi kufunga udhia wa mabao yake matatu.

Benzema alifunga bao la tano na kuiweka Real Madrid alama mbili nyuma ya viongozi Barcelona.