Mshindi wa Ballon d'Or kujulikana leo

Haki miliki ya picha d
Image caption Wachezaji watatu waliorodheshwa kushinda taji la mchezaji bora dunia mwaka 2015

Mmoja kati ya miyamba ya soka duniani,Lionel Messi,Christiano Ronaldo au Neymar huenda akatawazwa kuwa mshindi wa tuzo la Ballon d'Or,tuzo linalopewa mchezaji bora duniani.

Tuzo hiyo inayopigiwa kura na makocha wa kimataifa ,manahodha wa timu na waandishi litalowewa kwa mara ya 60 katika hafla ya kipekee mjini Zurich nchini Switzerland.

Kutoka Stanley Matthews aliyeshinda mwaka tuzo hilo mwaka 1956 hadi Christiano Ronaldo mwaka uliopita,washindi wake wameorodheshwa katika kipindi cha miaka 59 iliopita.

Katika miaka ya kombe la dunia asilimia 47 ya washindi wa tuzo hilo waliyasaidia mataifa yao kushinda kombe hilo ikiwemo Bobby Charlton mwaka 1966,Mchezaji wa Ufaransa Zinedine Zidane mwaka 1998 pamoja na nahodha wa timu ya Itali Fabio Cannavaro mwaka 2006.

Ni Asilimia 36 pekee waliosaidia mataifa yao kushinda kombe la bara Ulaya.