Klopp amuonya Guardiola kuhusu EPL

Haki miliki ya picha afp getty
Image caption Jurgen Klopp

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp, amemuonya Pep Guardiola kuwa changamoto kuu atakayokumbana nayo katika ligi kuu ya Uingereza, ni wingi wa mechi wanazocheza.

Guardiola, 44, ambaye anaihama klabu ya Bayern Munich mwisho wa msimu huu, amesema ana matarajio ya kufanya kazi nchini Uingereza.

Klopp, 48, amesema idadi ya mechi wanazocheza ni nyingi sana na imemshangaza sana. ''Wakati nilifika hapa sikujua kuna raundi mbili katika sem fainali ya kombe la Capital one.'' Alisema Klopp ambaye zamani alikuwa meneja wa klabu ya Borussia Dortmund.

Haki miliki ya picha All SPort
Image caption Pep Guardiola

Klopp amesema amepokea risala za heri njema kutoka kwa marafiki baada ya Liverpool kuishinda Stoke 1-0, katika mechi ya raundi ya kwanza na nusu fainali ya kombe la Ligi siku ya Jumanne.

Klopp, ambaye anafanya kazi nje ya Ujerumani kwa mara ya kwanza baada ya kuondoka Borussia Dortmund mwisho wa msimu uliopita, amesema ana sababu ya kuwa na matumaini makubwa akiwa Uingereza.