Jonjo ajiunga na Newcastle united

Image caption Jonjo Shelvey

Klabu ya soka ya Newcastle united imemsajili kiungo Jonjo Shelvey kutoka Swansea City.

Newcastle, wametumia kiasi cha pauni milioni 12 kumsajili kiungo huyu wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa 23.

Jonjo alifanikiwa katika vipimo vya afya na kusaini mkataba wa miaka mitano na nusu kukitumikia kikosi hicho cha Steve Mclaren.

Baada ya uhamisho huo kukamilika kocha mkuu wa kikosi cha Newcastle alimzungumzia mchezaji huyu na kusema "Ni mchezaji mwenye uzoefu katika viungo wa kati wa kiingereza.

Timu ya zamani ya Jonjo, Charlton,watapata kiasi cha mgao wa mchezaji huyo ambae alingara katika kiungo ya klabu ya Swansea msimu huu.