Newcastle kuchuana na Man United

Haki miliki ya picha AP
Image caption Man United ikichuana na Newcastle

Nahodha wa kilabu ya Newcastle Fabricio Coloccini ,winga Florian Thauvin na beki Kevin Mbabu huenda wasishiriki katika mechi ya ligi kuu Uingereza dhidi yao na Manchester United kutokana na majereha.

Hatahivyo,Midfielder Jack Colback anatarajiwa kurudi katika kikosi cha timu hiyo baada ya kupona jeraha.

Wakati huohuo kiungo wa kati wa Manchester United Bastian Scweinsteiger hatoshiriki katika mechi hiyo kutokana na jereha la goti alilopata wakati wa mchuano kati ya timu yake na Sheffield United.

Morgan Schneiderlin ,Michael Carrick na Ashley Young hawakushiriki katika mechi hiyo na huenda wakacheza.