Newcastle yatoshana nguvu na Man Utd

Georginio Wijnaldum Haki miliki ya picha PA
Image caption Georginio Wijnaldum alifungia Newcastle bao la kwanza

Newcastle United wakicheza katika dimba lao la St James Park wamekwenda sare ya kufunga mabao 3-3 na Manchester United.

Wayne Rooney alianza kuandikishia Man United bao la mapema kwa mkwaju wa penalti kisha kinda Jesse lingard akaongeza bao la pili katika dakika ya 38, katika dakika ya 42 kiungo Georginio Wijnaldum akaifungia Newcastle bao la kwanza.

Mshambuliaji Aleksandar Mitrovic akasawazisha bao la pili kwa upande wa timu yake kwa mkwaju wa penalti.

Rooney kwa mara nyingine aliweka Man Utd mbele kwa kuongeza bao la tatu. Lakini ikiwa imesalia dakika moja mpira kumaliza beki Paul Dummett alitikisa wavu na kufanyas mchezo kumalizika sare.

Wagonga nyundo wa London West Ham katika mechi nyingine wamechomoza na ushindi wa mabo 3-1 dhidi ya Bournemouth, Enner Valencia akifunga mabao mawili na Dimitri Payet akitupia moja huku bao la Bournemouth likifungwa na Harry Arter.

Aston Villa wamepata ushindi wao wa kwanza chini ya meneja Remi Garde kwa kuichapa Crystal Palace bao 1-0, bao lilofungwa na Joleon Lescott. Hata hivyo Villa wanaendela kuburuza mkia wakia na alama 11.