CHAN 2016:Rwanda yaichapa Ivory Coast

Haki miliki ya picha Other
Image caption Rwanda

Waandalizi wa michuano ya kombe la Afrika CHAN,Rwanda wameanza vyema kampeni yao baada ya kuifunga Ivory Coast 1-0.

Beki wa Rwanda Emery Bayisenge alifunga bao la kipekee katika dakika ya 15.

The Amavubi kama wanavyojiita walikuwa na fursa ya kufanya mambo kuwa 2-0 baada ya lisaa moja lakini kipa wa ndovu wa Ivory Coast Badra Ali Sangare alifanikiwa kuokoa hatari hiyo.

Image caption Sherehe za ufunguzi wa michuano hiyo

Lakini licha ya kukosa nafasi hiyo ya wazi ,Rwanda Rwanda ilijipatia alama muhimu mbele ya mashabiki wao wa Kigali.

Mchuano huo wa wachezaji wanaocheza barani Afrika pekee,ndio mchuno mkubwa kuwahi kuandaliwa na Rwanda.

Kinyang'anyiro hicho kinashirikisha timu 16 katika miji mitatu huku mji wa Kigali na ule wa Gisenyi huko Magharibi na Butare kusini ikiandaa mechi hizo.