MOJA KWA MOJA: Liverpool dhidi ya Man United

Timu ya liverpool inakabiliana na Manchester united katika mechi ngumu ya ligi kuu ya uingereza wikendi hii.

6.56pm:Na kipindi cha kwanza cha mechi chakamilika hapa ikiwa manchester United wameibuka kidedea kwa bao moja kwa nunge

6.53pm:Dakika tatu za lala salama zaongezwa

Image caption Wayne rooney

6.42pm:Goooooooal Wayne Rooney aiweka kifua mbele Manchester United mbele ya mashabiki wa Liverpool uwanjani Anfield

6.34pm:Liverpool yafanya mashambulizi kupitia Milner na sakho lakini mabeki wa manchester United wakataa

Haki miliki ya picha PA
Image caption Kocha wa Liverpool Jurgen Klop

6.34pm:Memphis Depay aingia Handers Herera atoka upande wa manchester united

6.29pm:La la la Kipa Degea aokoa mikwaju ya washambulizi wa Liverpool hapa na kuiepushia manchester United matatizo zaidi

6.27pm:Smalling apewa kadi ya njano kwa kumshika mshambuliaji wa Liverpool Firmino alipokuwa akielekea kushambulia lango la Manchester United.

Image caption Mashabiki wa Liverpool wakiimba uwanjani Anfield

6.22pm:Liverpool wavamia lango la man United kama chungu ambao wameona kivuno lakini Firmino anapiga mkwaju ,mpira unakuwa mwingi na unapaa juu ya goli la United

6.19pm:Wachezaji wa Man United wainua mikono hapa wakidhani kwamba huenda wakapewa penalti baada ya mchezaji wao kuangushwa lakini refa anasema ngome iendelee

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wayne Rooney

Manchester United washambulia hapa hatari! hatari !Martial apiga nje lo lo...Liverpool yaponea chupuchupu.

6.14pm:Liverpool waendelea kulishambulia lango la United lakini bahati haijasimama.Liverpool yapata kona lakini yatoka.

6.00pm:Kipindi cha pili cha mechi chaanza.

5.45pm:Na kipindi cha kwanza cha mechi chakamilika ikiwa Liverpool 0-0 Manchester United

Image caption Liverpool dhidi ya manchester United

5.36pm:Liverpool waimiminia timu ya Manchester United mashambulizi baada ya mashambuliza,ijapokuwa bahati haijasimama.

5.30pm:WACHEZAJI WA MANCHESTER UNITED:

01 de Gea18 Young12 Smalling17 Blind36 Darmian28 Schneiderlin27 Fellaini35 Lingard21 Herrera09 Martial10 Rooney

Wachezaji wa ziada

07 Depay08 Mata20 Romero30 Varela33 McNair43 Borthwick-Jackson44 Pereira

Ref: Mark Clattenburg

Image caption Mechi yapamba moto

5.29Pm:Mechi yapamba moto huku Manchester United wakionyesha ari yao ya kutaka kushinda mechi

5.28pm:WACHEZAJI WA LIVERPOOL:

22 Mignolet02 Clyne04 K Touré17 Sakho18 Moreno14 Henderson21 Lucas23 Can07 Milner11 Firmino20 Lallana

Wachezaji wa ziada

09 Benteke19 Caulker24 Allen33 Ibe44 Smith52 Ward53 J. Teixeira

5.25pm:CHAN:Kipindi cha kwanza kimemalizika.Congo wanaongoza kwa goli 1-0 dhidi ya Ethiopia lililopatikana kwenye dakika ya 44 mfungaji Lusadisu

5.21pm:Nguvu nyingi zinatumika katika mechi hii huku baadhi ya wachezaji wakionywa na refa kwa kucheza rafu

Image caption Liverpool dhidi ya manchester United

5.16pm:Ni mechi inayochezwa kwa kasi ya hali ya juu huku liverpool ikiendelea na mfumo wake wa pasi ndefu.

5.15pm:Liverpool yafanya mashambulizi kupitia lalana na firmino lakini Manchester United waipuka

17.10pm:Manchester United yaanza kwa kasi ya juu hapa ikiwa wachezaji wa Liverpool wanalazimaika kurudi nyuma ili kulinda lango lao.

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Kocha Louis Van Gaal

5.00pm:Mechi kati ya Liverpool na manchester United yaanza katika uwanja wa Anfield.