Van Gaal:Bado tuna fursa ya kushinda ligi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Van Gaal

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa kilabu yake bado ina fursa ya kushinda ligi ya Uingereza.'

Mshetani wekundu' kama wanavyojiita waliishinda Liverpool 1-0 katika uwanja wa Anfield siku ya jumapili na kupanda hadi nafasi ya tano katika jedwali la ligi hiyo,wakiwa pointi saba pekee nyuma ya viongozi wa ligi hiyo Arsenal na Leicester ilio nafasi ya pili.

''Kuna mechi nyingi ambazo zimesalia'',alisema Van Gaal alipoulizwa iwapo timu yake itapigania taji hilo.

''Ni lazima tuendelee'',ijapokuwa si rahisi,lakini tunaweza kufanikiwa kwa sababu tunaonyesha kila wiki kwamba tunaweza''.

United ilipunguza mwanya uliopo kati yake na viongozi wa ligi hiyo Arsenal na Leicester baada ya timu hizo mbili kupata droo, ijapokuwa Manchester City iliopo katika nafasi ya tatu pamoja na Tottenham iliopo nafasi ya nne.