Nadal ashindwa raundi ya kwanza Australia

Nadal Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nadal alishindwa seti tano

Rafael Nadal ameondolewa kwenye raundi ya kwanza katika shindano la tenisi la Australian Open baada ya kushindwa seti tano na Fernando Verdasco.

Hii ni mara ya kwanza kwa Nadal kuondolewa kwenye shindano katika raundi ya kwanza.

Wachezaji hao wawili kutoka Uhispania, wanaotumia mikono ya kushoto, walikabiliana katika uwanja wa Rod Laver Arena kwa zaidi ya saa nne na dakika 40.

Verdasco alishinda 7-6 (8-6) 4-6 3-6 7-6 (4-7) 6-2.

Mwanatenisi huyo aliyeorodheshwa nambari 45 duniani sasa atakutana na Dudi Sela kutoka Israel raundi ya pili.

Haki miliki ya picha AP

“Nilicheza vyema sana raundi ya tano. Sijui nilifanikiwa vipi. Nilifunga macho yangu na kila kitu kikawa sawa,” amesema Verdasco, 32.

Verdasco alishindwa na Nadal nusufainali za 2009.