CHAN: Rwanda yafuzu robofainali

Rwanda
Image caption Mechi ya mwisho Rwanda watakutana na Morocco tarehe 24 Januari

Rwanda imekuwa timu ya kwanza kufuzu kwa robofainali ya michuano ya taifa bingwa Afrika kwa wachezaji wa ndani baada ya kuilaza Gabon.

Rwanda, ambao ni wenyeji, wameandikisha ushindi wa 2-1 dhidi ya Gabon, kwenye mechi hiyo iliyochezewa uwanja wa Amahoro.

Mabao ya Rwanda yamefungwa na Sugira Ernest, la kwanza mwishoni mwa kipindi cha kwanza na la pili mapema kipindi cha pili.

Rwanda ilifungua michuano hii kwa kucharaza Ivory Coast, ambao watakutana na Morocco baadaye leo, mabao 1 -0.