CHAN: Uganda watoka sare na Mali

Uganda
Image caption Uganda watakutana na Zambia Jumamosi

Mali walitoka nyuma mara mbili na kulazimisha sare ya 2-2 mechi ya taifa bingwa Afrika kwa wachezaji wa ndani kati yao na Uganda.

Mechi hiyo ilichezewa mjini Rubavu, Rwanda.

Kwenye mechi nyingine ya Kundi D, Zambia waliwanyuka majirani zao Zimbabwe 1-0.

Nahodha wa Uganda Farouk Miya alisaidia kufunga bao la kwanza na kisha akawafungia bao la pili kabla ya kuondolewa wakati wa mapumziko baada ya kuumia.

Bao la kwanza la Uganda lilifungwa kwa kichwa naJoseph Ochaya kipindi cha kwanza.

Mali walisawazisha dakika 12 baadaye kupitia Sekou Koita.

Dakika nne kabla ya mapumziko, Miya aliwafungia Uganda bao la pili kupitia mkwaju wa penalti baada ya Erisa Ssekisambu kuchezewa visivyo.

Uganda chini ya kocha Milutin 'Micho' Sredojevic hata hivyo walipata pigo Miya alipoumia na kushindwa kurejea kwa kipindi cha pili.

Kipa wao Watenga pia aliumia na msaidizi wake Mathias Kigonya akaingia nafasi yake.

Mali walisawazisha kupitia mshambuliaji Hamidou Sinayoko baada yake kupata pasi kutoka kwa Mamadou Coulibaly.

Mechi zijazo katika Kundi zitachezwa Jumamosi, Zimbabwe dhidi ya Mali nao Uganda wakabili Zambia.