CHAN: DR Congo yaichapa Angola

Congo
Image caption DR Congo walilaza Ethiopia 3-0 mechi ya kwanza

Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeandikisha ushindi wa pili michuano ya taifa bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani inayoendelea Rwanda.

DR Congo wamewalaza Angola 4-2 na sasa wanaongoza katika Kundi B na alama sita.

Angola wanashika mkia wakiwa bila alama yoyote.

DR Congo walikuwa wamepata uongozi wa 3-0 kupitia mabao ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Nelson Munganga, Elia Meschak na Jonathan Bolingi.

Gelson na Yano walikomboa mawili upande wa Angola, lakini hapo katikati Merveille Bope aliongezea DR Congo bao la nne.

Baadaye Alhamisi, Cameroon watakuwa wakisaka ushindi watakapokutana na Ethiopia ambao walilazwa 3-0 mechi yao ya kwanza na DR Congo.