Man United 'kuongoza kwa mapato duniani'

Man Utd Haki miliki ya picha Getty
Image caption Manchester United kwa sasa inashikilia nafasi ya tatu

Klabu ya Manchester United huenda ikawa klabu itakayokuwa ikipokea pesa nyingi zaidi duniani katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

Kwa mujibu wa orodha ya mapato ya klabu iliyotayarishwa na kampuni ya Deloitte, miamba wa Uhispania Real Madrid kwa sasa wanaongoza kwa mwaka wa 11 mtawalia.

Klabu hiyo ilipata euro 577m (£439m) msimu wa 2014-15.

Mabingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Barcelona wanashikilia nafasi ya pili wakiwa na euro 560.8m (£426.6m), huku United wakiwa nambari tatu kwa kujipatia euro 519.5m (£395.2m).

Lakini Deloitte wamesema kuna uwezekano mkubwa sana kwamba United huenda wakawa wamewapita Real Madrid wakati wa kutolewa kwa orodha ijayo.

Manchester United walishuka kutoka nambari mbili hadi nambari tatu baada ya kushuka kwa mapato yao lakini Deloitte wanasema “ukuaji thabiti wa kibiashara” wa Manchester United, pamoja na “uwezo wa kupata mikataba ya thamani kubwa ya uthamini” kama ule wa Adidas wa £75m kila mwaka, vimesaidia sana klabu hiyo.

Kutokana na mkataba mpya wa haki za utangazaji katika runinga wa thamani ya £5.1bn utakaoanza msimu wa 2016-17, Real Mdrid huenda ikatatizika kupata mapato ya juu.

Ligi ya Premia inaongoza kwa kuwa na klabu nyingi kwenye orodha ya klabu 30 tajiri, ikiwa na klabu 17.

Hii inatokana na mikataba mizuri ya utangazaji na upeperushaji wa mechi.

West Ham wamefika kwenye 20 bora kwa mara ya kwanza tangu 2005-06, baada ya kupata mapato ya euro 160.9m (£122.4m).

Manchester United waliongoza orodha hiyo, ambayo kwa Kiingereza hujulikana kama Deloitte Football Money League, ilipozinduliwa mwaka 1998, walipoandikisha mapato ya jumla ya £87.9m.

Orodha ya klabu kwa mapato kwa mujibu wa Deloitte

Nafasi mwaka huu (mwaka jana) Klabu Mapato ya 2014/15 (euro m) (Mapato ya 2013/14) Mapato ya 2014/15 (£m) (Mapato ya 2013/14)
1 (1) Real Madrid 577 (549.5) 439 (459.5)
2 (4) FC Barcelona 560.8 (484.8) 426.6 (405.4)
3 (2) Manchester United 519.5 (518) 395.2 (433.2)
4 (5) Paris Saint-Germain 480.8 (471.3) 365.8 (394.1)
5 (3) Bayern Munich 474 (487.5) 360.6 (407.7)
6 (6) Manchester City 463.5 (416.5) 352.6 (348.3)
7 (8) Arsenal 435.5 (359.3) 331.3 (300.5)
8 (7) Chelsea 420 (387.9) 319.5 (324.4)
9 (9) Liverpool 391.8 (305.9) 298.1 (255.8)
10 (10) Juventus 323.9 (279) 246.4 (233.3)
11 (11) Borussia Dortmund 280.6 (261.5) 213.5 (218.7)
12 (13) Tottenham Hotspur 257.5 (215.5) 195.9 (180.2)
13 (14) Schalke 04 219.7 (214) 167.1 (179)
14 (12) AC Milan 199.1 (249.7) 151.5 (208.8)
15 (15) Atletico de Madrid 187.1 (169.9) 142.3 (142.1)
16 (New) AS Roma 180.4 (127.4) 137.2 (106.5)
17 (19) Newcastle United 169.3 (155.1) 128.8 (129.7)
18 (20) Everton 165.1 (144.1) 125.6 (120.5)
19 (17) Internazionale 164.8 (162.8) 125.4 (136.1)
20 (New) West Ham United 160.9 (139.3) 122.4 (116.5)