Man United yalazwa,Liverpool yanusurika

Haki miliki ya picha AP
Image caption Manchester United

Mchezaji wa ziada Charlie Austin alifunga dakika saba baada ya kuingia na kuijeruhi Manchester United.

Manchester United na meneja wao Louis Van Gaal walizomwa na mashabiki baada ya timu hiyo kushindwa kufanya mashambulizi yoyote katika dakika 90.

Wakati huohuo Adam Lallana alifunga bao la dakika za lala salama na kuiwezesha Liverpool kuishinda Norwich City 5-4 katika mechi iliojaa mashambulizi msimu huu.

Haki miliki ya picha reuters
Image caption Liverpool

Robert Firmino aliiweka kifua mbele Liverpool lakini bao la kisigino la Dieumerci Mbokani lilisawazisha kabla ya bao La Steve Naismith kuiweka mbele Norwich

Wes Hoolan alifunga bao la penalti kwa upande wa wenyeji kabla ya Jordan Henderson na Frimino kusawazisha.

James Milner aliiweka Liverpool kifua mbele huku Sabastian Basson akisawazisha lakini Lallana akafunga bao la Ushindi.