Uwanja wa Mombasa:Eneo la kukimbilia laimarishwa

Image caption Ujenzi wa uwanja wa Mombasa

Ujenzi wa eneo la kukimbilia katika uwanja wa kaunti ya Mombasa nchini Kenya umeanza.

Mkurugenzi wa kampuni inayotekeleza ujenzi huo Bakar Agenzy Consultant, Abdinoor Maalim amesema kuwa uchimbaji wa eneo hilo tayari unaendelea vyema.

Image caption Abdinoor Maalim

Naibu mkurugenzi wa michezo nchini Kenya anayesimamia maswala ya kiufundi Wilberforce Chebet amesema kuwa mradi huo ni kupitia ushirikiano na kaunti ya Mombasa.

''Pia tuna mpango wa kuimarisha eneo la kuketi ili kuongeza idadi ya mashabiki.Tukimaliza mradi huu tutaweza kuandaa mashindano makubwa ya riadha kwa sababu Mombasa ina hoteli za kutosha kwa wageni''.

Image caption Ujenzi wa uwanja wa Mombasa

Wakati huohuo mipango kuhusu ujenzi wa uwanja mkubwa wa michezo mbalimbali katika eneo la Shanzu pembezoni mwa mji wa Mombasa Inaendelea.