Rais Ashraf Ghani,ataka mazungumzo

Haki miliki ya picha epa
Image caption Rais wa Afghanstan Ashraf Ghani

Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani, ametoa onyo kwamba endapo mazungumzo ya kutafuta amani baina ya nchi yake na Taliban hayatafanikiwa kuanza mpaka kufikia mwezi April, ulimwengu utarajie mgogoro baina yao utazidi kukua.

Rais Ashraf amesema kwamba suala hilo linaweza kukua na kugubika kanda yake,akizungumza na BBC, Rais Ghani ameitaka nchi ya Pakistan kuungana na nchi yake kukabiliana na vitendo vya kigaidi.

Majeshi ya waasi yanasonga mbele kufikia mpaka na nchi ya Pakistan mahali ambako nchi zote mbili zinalengwa na mashambulizi.Ghan pia ametoa wito wa mapambano dhidi ya uwepo kundi la kigaidi lenye mbinu la Islamic State katika nchi yake.