Konta kuandika historia Australia Open

Image caption Johanna

Mwingereza Johanna Konta anaweza kuandika historia ya kuwa mcheza tenesi wa kwanza Mwingereza toka mwaka 1984 kutinga hatua ya nufu fainali ya Grand Slam katika michuano ya wazi ya Australia .

Nyota huyu anayeshika nafasi ya 47 kwa ubora wa viwango duniani atashuka dimbani leo hii kuchuana na Ekaterina Makarova

Konta mwenye umri wa miaka 24 atakua na kibarua kizito kuweza kuandika historia mpya.

Mwaka 1984, Mwingereza Jo Durie, alifika hatua ya nane bora katika michuano ya wazi ya Wimbledon' na hakuna mchezaji wa tenesi wa kike wa Uingerza amewahi kufika hatua hiyo ya nane bora.