Murray,Konta watinga robo fainali

Image caption Johanna Konta

Nyota Johanna Konta amekua mchezaji wa kwanza wa kike wa Uingereza kufanikiwa kutinga hatua ya robo ya Grand Slam ikiwa ni miaka 32 toka alipofanya hivyo Jo Durie.

Konta alipata ushindi dhidi ya Mrusi Ekaterina Makarova kwa jumla ya seti 4-6 6-4 8-6, Mwingereza wa mwisho kufika robo fainali ya Grand Slam alikue ni Jo Durie, aliyefika hatua hiyo katika michuano ya Wimbledon ya mwaka 1984.

Nae Andy Murray akasonga mbele kwenye hatua ya nane bora kwa kumshinda mpinzani wake Bernard Tomic.

Murray alipata ushindi wa seti 6-4 6-4 7-6 (7-4).Hatua ya robo fainali kwa upande wa wanaume itawakutanisha

Novak Djokovic na Kei Nishikori Roger Federer na Tomas Berdych

Gaels Monfils na Milos Raonic David Ferrer na Andy Murray

Robo fainali kwa upande wa wanawake

Serena Williams na Maria Sharapova, Agnieszka Radwanska na Carla Suarez Navarro

Angelique Kerber na Victoria Azarenka ,Johanna Konta na Shuai Zhang