Urusi yawafungia wanariadha wake wanne

Image caption Irna Maracheva

Kamati ya Olimpiki ya Urusi (Roc) imewafungia wanariadha wanne kwa tuhuma za matumizi ya kutumia dawa za kusisimua misuli michezo.

Waliofungiwa ni pamoja na mshindi wa medali ya fedha wa mashindano ya ulaya Irina Maracheva aliyefungiwa kwa muda wa miaka miwili.

Mkimbiza upepeo mwingine aliyefungiwa ni Anna Lukyanova ambae pia amefungiwa kwa miaka miwili kutojihusisha na mchezo huo.

Kamati ya Olimpic pia imewasimamisha Maria Nikolaeva na Yelena Nikulina kwa muda wa miaka minne kutoshiriki mchezo wa riadha.