Liverpool yatinga fainali ya Capital One

Haki miliki ya picha Getty

Wakicheza nyumbani kwao Anfield Liverpool wameshinda mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe la Capital One dhidi ya Stoke na kutinga fainali.

Majogoo hao wa Anfield walipata ushindi wa mabao 6-5 kwa mikwaju ya penati baada dakika tisini kumalika kwa Liverpool kufungwa bao 1-0, bao lilofungwa Marko Arnautovic hivyo kuufanya mchezo huo kuwa sare baada ya Liverpool kushinda kwa 1-0.katika nusu fainali ya kwanza.

Beki Marc Muniesa ndie aliyekosa penati ya mwisho ya Stoke baada ya kuokolewa na kipa Simon Mignolet, huku kiungo Joe Allen akifunga penati ya mwisho ya ushindi.

Liverpool wanasubiri mshindi wa mchezo mwingine wa nusu fainali unachezwa leo kati ya Man City wataokua katika uwanja wao wa Etihad wakiwalika Everton. Huku Everton wakiwa wanaongoza kwa ushindi mabao 2-1 mabao yaliyapata katika mchezo wa kwanza.