Serena amtambia Sharapova

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Serena Williams akiwajibika

Nyota wa tenesi Serena Williams ameendelea kumtambia Maria Sharapova baada ya kumshinda katika michuano ya wazi Australia.

Huu ni ushindi wa kumi na nane mfululizo kwa Serena dhidi ya Sharapova, na kwa ushindi Serena anasonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali.

Bingwa huyu wa mtetezi taji hilo akilisaka taji la 22 la Grand Slam alipata ushindi wa seti 6-4 6-1 mchezo ulifanyika katika uwanja wa Melbourne Park.

Imepita miaka 12 tangu nyota huyu wa Marekani alipopoteza mchezo dhidi ya Sharapova,Serena atachuana na Agnieszka Radwanska katika hatua ya nne bora.