Tenisi: Murray na Konta watinga nusu fainali

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Tenisi: Murray na Konta watinga nusu fainali

Uingereza imeandikisha rekodi ya kuwa a wachezaji wawili katika hatua ya nusu fainali ya mashindano ya tenisi ya Grand Slam kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1977.

Wachezaji wawili wa Britain Johanna Kontana Andy Murray walivunja rekodi hiyo baada ya kutinga hatua ya nusu Fainali ya mchuano wa tenisi ya wazi ya Australia.

Konta alikuwa wakwanza kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kumzima mpinzani wake Zhang Shuai kutoka China seti mbili kwa nunge za alama 6-4 6-1 .

Kufuatia ushindi huo mkubwa Konta sasa ameratibiwa kuchuana dhidi ya Mjerumani Angelique Kerber anayeorodheshwa katika nafasi ya 7 bora duniani.

Image caption Konta alikuwa wakwanza kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kumzima mpinzani wake Zhang Shuai kutoka China seti mbili kwa nunge

Konta ambaye ameorodheshwa katika nafasi ya 47 duniani alihitaji muda wa saa moja na dakika 22 kuandikisha jina lake katika daftari za kihistoria.

Konta sasa amekuwa mwanamke wa kwanza raia wa Uingereza kufuzu kwenye hatua ya nusu fainali tangu Jo Durie mwaka wa 1983.

Aidha Muingereza huyo sasa anatarajiwa kutia kibindoni takriban pauni £370,000 mbali na kuimarika hadi nafasi ya 30 bora duniani.

Wakati huo Muingereza anayeorodheshwa katika nafasi ya pili duniani Andy Murray alijikatia nafasi ya nusu fainali baada ya kumtupa nje David Ferrer seti tatu kwa moja za alama 6-3 6-7 (5-7) 6-2 6-3

Hii ikiwa ndiyo nusu fainali yake ya 6 mjini Melbourne Murray ameratibiwa kuchuana dhidi ya mshindi kati ya Gael Monfils na Milos Raonic Ijumaa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Murray alijikatia nafasi ya nusu fainali baada ya kumtupa nje David Ferrer seti tatu kwa moja

Murray, 28, alihitaji muda wa saa tatu na dakika 49 kumnyamazisha mpinzani wake anayeorodheshwa wa nane bora duniani.

Aidha kufuatia ushindi wake Murray ametoshananguvu na mchezaji aliyetamba miaka ya awali katika mchezo huo Boris Becker.

Becker alifuzu katika mashindano 18 ya Grand Slam .