Griffin wa Los Angeles aomba radhi

Image caption Blake Griffin

Nyota wa mpira wa kikapu Blake Griffin wa timu ya Los Angeles Clippers ameomba radhi kwa kushiriki tukio la ugomvi.

Ugomvi huo ulimpelekea Griffin kuvunjika mkono wa kulia na hivyo atakaa nje ya dimba kwa muda wa wiki nne mpaka sita kuuguza mkono huo.

NBA wanachunguza tukio hilo, ambao ulilitokea siku ya Jumamosi nje ya mgahawa wa Toronto ,Griffin ambae ni nyota wa timu ya All Star kwa mara tano alivunjika mkono wakati akizua konde la vifaa kutoka kwa meneja wa vifaa wa Los Angeles Clippers.

Griffin ameeleza" nataka kuomba radhi kwa taasisi ya Clippers,wachezaji wenzangu na mashabiki. Nafanya kazi na timu na nitarudi kwenye mchezo haraka iwezekanavyo.