Man City kuchuana na Liverpool fainali

Haki miliki ya picha Getty

Man City imekua timu ya pili kufuzu fainali ya mchezo wa kombe la Capital baada ya kuichapa Everton kwa mabao 3-1.

Everton ndio walikua wa kwanza kuzifuma nyavu za Man City baada ya kiungo Ross Barkley kuifungia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 18 ya mchezo.

Kiungo kutoka Brazil Fernandinho akasawazisha bao hilo kwa shuti kali baada ya kutoka piga nikupige kwenye goli la everton katika dakika ya 25.

Kevin De Bruyne akaongeza bao la pili baada ya kunganisha krosi ya kutoka upande wa kushoto iliyopigwa na Raheem Sterling, kisha Sergio Aguero kun, akahitimisha kazi kwa bao la tatu.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Goodson Park Everton walishindwa kwa ushindi wa mabao 2-1.

Man City watachuana na Liverpool katika mchezo wa fainali utaofanyika Februari 28 katika dimba la Wembley.