Mwenyekiti wa FA Dyke kung'atuka june

Haki miliki ya picha PA
Image caption Greg Dyke

Mwenyekiti wa chama cha soka cha England FA Greg Dyke atajiengua kwenye wadhifa huo mwezi june,mwaka huu baada ya muda wake kumalizika.

Kwa mujibu wake Dyke hatogombea tena nafasi hiyo,ambayo alichaguliwa mwaka 2013 na amekitumika chama cha soka kwa muda wa miaka mitatu.Na alikua na lengo la kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Wakati Dyke akichukua uongozi toka kwa David Bernstein,alisema England inapaswa fika nusu fainali ya Euro 2020, na kutwaa kombe la dunia mwaka 2022.

Mwenyekiti huyu alitoa maelezo katika mkutano wa bodi ya chama cha FA ilipokutana katika uwanja wa Wembley na akaeleza " kama mnavyofahamu mapema mwezi January nilitangaza nitaendelea kuwa mwenyekiti kwa mwaka mmoja zaidi ila nafikiri yale hayakua maamuzi sahihi.