Virusi vya Zika havitaathiri Olimpiki, kamati yasema

Haki miliki ya picha AP
Image caption Margaret Chan mkurugenzi mkuu wa WHO

Mamlaka ya mashindano ya kimataifa ya Olimpiki imesema itafanya kila iwezalo ili kulinda usalama wa michezo hiyo itakayofanyika Rio de Janero wakati ambapo kuna maambukizi ya virusi vya Zika.

Ikiwa Brazil ndio nchi iliyoathirika zaidi na virusi hivyo vya zika,kiongozi wa mashindano hayo ya Olimpiki,Thomas Bach alisema mapendekezo ya namna gani wachezaji na wageni watakuwa salama itafanyiwa kazi wiki hii.

Mbu hawa wanaoambukiza virusi vya zika wanaaminika kuwa wanaathiri kizazi cha mtoto kabla hajazaliwa,shirika la afya duniani ametoa onyo kuwa ugonjwa huu unasambaa kwa kasi.Msemaji wa shirika hilo la afya, Marcos Espinal anasema kuna kesi milioni nne za zika kusambaa nchini marekani mpaka mwakani,wakiwa wanalinganisha na maambukizi ya homa ya dengue (kidingapopo).

Thomas Bach Rais wa Kamati ya Olimpiki duniani amewaambia waandishi wa habari kuwa wanafanya kazi na Shirika la Afya duniani kuhakikisha usalama wote watakaohudhuria mashindano hayo mwezi Agosti.

Thomas anasema: "Kuhusu suala la virus hivi, tunafanya kazi kwa karibu na shirika la Afya duniani WHO, pamoja na kamati maaandalizi pamoja na mamlaka nchini Brazil. Unafahamu kwamba Rais wa Brazil Dilma Rousseff ameitisha mkutano wa marais."

"Kuna mkutano wa marais wa nchi za Amerika ya kusini kwa ajli ya jambo hili lakini kwa hivi sasa mawaziri wa afya wa eneo hilo wanakutana kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.Pia tunatarajia mashindano ya olimpiki yatafanyika wakati wa majira ya baridi, hivyo kwa wakati huo kutakuwa na hali ya hewa tofauti na ya hivi sasa wakati ambapo ni wakati wa majira ya joto huko Brazil."