CHAN2016:Rwanda kumenyana na DR Congo

Haki miliki ya picha Other
Image caption Rwanda

Waandalizi wa michuano ya CHAN2016 Rwanda hii leo wanamenyana na DR Congo katika mechi kali ya robo fainali ya kwanza ili kuweza kufuzu kwa semi fainali.

Kikosi hicho cha Amavubi kilifuzu katika robo fainali baada ya kuishinda Ivory Coast 1-0 katika mechi ya ufunguzi ,na kupata ushindi mwengine wa 2-1 dhidi ya Gabon.

Na licha ya kushindwa 4-1 na Morocco katika mechi ya mwisho ya kimakundi,walimaliza kama washindi wa kundi A.

Haki miliki ya picha Other
Image caption DR Congo

Lengo lao hatahivyo halitaafikiwa kwa urahisi kwa kuwa wanakabiliana na chui wa DR Congo ambao wana safu bora ya mashambulizi katika michuano hiyo pamoja na Tunisia baada ya kufunga mabao 8.

DR Congo walianza kampeni yao ya michuano hiyo kwa kupata ushindi mzuri dhidi ya Ethiopia na baadaye kuicharaza Agola 4-2 kabla ya kushindwa na Cameroon 1-3 ambao walipanda katika kilele cha Kundi B na pointi 7,wakiwa pointi moja juu ya chui hao waliokuwa katika nafasi ya pili.