Mjerumani Kerber amshangaza Serena

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kerber amshinda Serena

Mjerumani Angelique Kerber, amemshinda Serena Williams katika mashindano ya tennis ya wanawake ya Australian Open.

Haya ndio mashindano ya mwanzo makubwa kwa Kerber kushiriki.

Kwa kushinda, amemenyima ushindi Williams, ambaye angelishinda, angekuwa na rikodi sawa na mwanamke mwengine wa Ujerumani, Steffi Graf, ambaye rikodi yake ya ya kushinda mechi kuu 22, haikuvunjwa tangu mwaka 1999.