Anaswa na injini katika mashindano ya baiskeli

Haki miliki ya picha
Image caption Anaswa na injini katika mashindano ya baiskeli

Shirikisho la kudhibiti mashindano ya mbio za baiskeli, linachunguza iwapo mshiriki mmoja wa mbio hizo alitumia baiskeli yenye mota (Injini ndogo) katika mashindano.

Chama cha UCI kimenasa baiskeli moja iliyotumika katika mbio za wanawake wenye chini ya umri wa miaka 23, katika mashindano ya uendeshaji baiskeli nchini Ubelgiji.

Mwendeshaji baiskeli hiyo Femke Van den Driessche alikuwa amepigiwa upatu kuibuka mshindi wa mashindano hayo lakini akajiondoa kufuatia matatizo ya baiskeli.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bi Van den Driessche amekanusha madai dhidi yake anasema baiskeli hiyo inamilikiwa na rafiki yake.

Bi Van den Driessche amekanusha madai dhidi yake anasema baiskeli hiyo inamilikiwa na rafiki yake.

Rais wa Shirikisho la mashindano ya baiskeli- UCI, Brian Cookson anasema kuwa mshukiwa sio miongoni mwa washindi watatu wa kwanza katika mashindano hayo.

Ikiwa udanganyifu huo utathibitishwa , itakuwa kisa cha kwanza kabisa kutambuliwa kama "udanganyifu wa kiufundi'' kuwahi kutokea katika mashindano ya baiskeli..

Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, waendesha baiskeli wamechunguzwa kwa kutumia baiskeli zilizo na injini ndogo (motor) zilizofichwa katika mashindano makubwa ya baiskeli.