Newscastle wamtafuta Saido Berahino

Saido Haki miliki ya picha PA
Image caption Berahino alishindwa kuhamia Spurs Agosti mwaka jana

Newcastle United wamewasilisha ombi la £21m la kutaka kumnunua mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino.

Meneja wa West Brom Tony Pulis alisema Berahino, 22, “amepoteza miezi mitatu au mme” baada yake kuzuiwa kuhamia Tottenham Agosti mwaka uliopita.

Mshambuliaji huyo alionekana kusema kwamba hangechezea mwenyekiti wa West Brom Jeremy Peace tena baada yake kuzuiwa kuhama.

Berahino alianza mechi, jambo ambalo limekuwa nadra sana kwake, mechi dhidi ya Peterborough katika Kombe la FA Jumamosi na akawafungia mabao mawili na kuwasaidia kutoka sare ya 2-2.

Mabao hayo yalifikisha jumla ya mabao aliyofunga msimu huu hadi sita.

Msimu uliopita, amefungia West Brom mabao 22 ligini kwa jumla.

"Kuna siku nyingine mbili za kusubiri,” alisema Pulis baada ya mechi dhidi ya Peterborough Jumamosi.

Muda wa kuhama wachezaji utamalizika leo usiku, na iwapo atafanikiwa kuhama, basi West Brom hawatakuwa na muda mwingi wa kutafuta mchezaji wa kujaza nafasi yake.