Wajawazito kukosa Olimpiki Brazil

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanawake wajawazito wameshauriwa kutosafiri kwenda Rio de Jeneiro wakati wa michezo ya Olimpiki

Wanawake wajawazito wameshauriwa kutosafiri kwenda Brazil kushuhudia mashindano ya Olimpiki mwaka 2016 kwa sababu ya hatari ya virusi vya Zika.

Serikali ya Brazil imesema kuwa hawashauri wanawake wajawazito kwenda kwenye michezo ya Olimpiki jijini Rio De Jeneiro mwezi Agosti

hatua hii imekuja punde baada ya shirika la afya duniani WHO kutangaza hali ya dharura kutokana na madhara yatokanayo na virusi vya Zika.