Guardiola kuwa meneja Manchester City

Pep Haki miliki ya picha All SPort
Image caption Guardiola kwa sasa ni meneja wa Bayern Munich ya Ujerumani

Mhispania Pep Guardiola ametia saini mkataba wa miaka mitatu kuwa meneja mpya wa Manchester City baada ya msimu huu kumalizika.

Guardiola, atachukua majukumu hayo kuanzia Julai, klabu hiyo ya Ligi ya Premia imetangaza.

Manuel Pellegrini ataondoka klabu hiyo Juni 30 baada ya kumalizika kwa msimu wa sasa.

"Kutokana na heshima yetu kwa Manuel Pellegrini na wachezaji, klabu ingependa kufanya wazi uamuzi wake ili kuondoa nafasi ya uvumi,” City wamesema kupitia taarifa kwenye tovuti yao.

Manchester City imekamilisha majadiliano na Pep Guardiola na sasa imeshatia sahihi kandarasi na kocha huyo kuchukua hatamu msimu ujao wa 2016/17

Manchester City

"Manuel, ambaye anaunga mkono kikamilifu uamuzi wa kufanya tangazo hili, anaangazia kutimiza malengo yake ya msimu huu na anadumisha kujitolea na heshima ambayo amekuwa nayo machoni ma wote wanaohusika katika uongozi wa klabu.”