BBC kutangaza michuano ya Olimpiki

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Michezo ya BBC kutangazwa kwenye redio,televisheni na mtandaoni

Shirika la utangazaji la BBC limepata haki ya kupeperusha matangazo ya michezo ya Olimpiki hadi majira ya joto mwaka 2024.

Hata hivyo haitaweza kupeperusha kila kitu moja kwa moja sawa na ilivyofanyika kwa michezo ya London 2012.

Shirika hilo limekubali kulipia leseni ya kupeperusha michezo hiyo kwenye televisheni na pia mtandaoni kutoka kwa kampuni ya Discovery Communications kwa ajili ya michezo ya majira ya baridi ya 2022 na majira ya joto ya 2024.

Msemaji mmoja wa BBC amesema shirika hilo litakuwa likichangua ni michezo gani ya kuonyesha kupitia chaneli mbili za televisheni.

Mtandaoni pia, kutakuwa na aina mbili za matangazo.

Mkurugenzi mkuu wa BBC Tony Hall amesema: "BBC inajivunia kutangazia umma matukio ya kusisimua ya michezo hii muhimu. Kwa wengi, BBC imekuwa ndiyo uwanja wao ambapo huwa wanatazama na kufuatilia mashindano. Ni mashindano yanayounganisha taifa.Nina furaha kwamba kupitia ushirikiano wetu na Discovery, BBC itaendelea kupeperusha mwenye wa kuangazia michezo vyema zaidi hadi Michezo ya 2024.”

Discovery ndiyo inayomiliki haki zote za matangazo ya michezo hiyo Ulaya hadi 2024 baada ya kuingia kwenye mkataba na Kamati ya Olimpiki.