Dirisha la uhamisho lakamilika Uingereza

Image caption wakufunzi wa vilabu vya ligi ya Uingereza.

Stoke na Everton zilikamilisha mikataba ya uhamisho wa wachezaji na hivyobasi kuongeza matumizi ya dirisha la uhamisho mwezi Januari kufikia pauni milioni 175.

Vilabu vya ligi ya Uingereza vimetumia pauni bilioni 1.045 katika dirisha la uhamisho katika msimu wa 2015-2016.

Stoke ilivunja rekodi ya uhamisho kwa kumnunua Gianelli Imbula kwa pauni milioni 18.3,huku Everton ikitumia pauni milioni 13.5 kumnunua mshambuliaji wa Lokomotiv Moscow Oumar Niasse.

Rekodi iliokuwepo ya matumizi miongoni mwa kilabu hizo ilikuwa pauni milioni 965 katika msimu wa 2014-2015.

Image caption Matumizi ya ligi tofauti msimu huu

Mtaalam wa maswala ya kifedha kutoka kampuni ya Deloitte, Dan Jones alisema: Matumizi haya ya Januari yameshinikizwa kwa kiasi kikubwa na vilabu vilivyopo chini ya jedwali la ligi ya Uingereza'.

Mkataba mpya wa matangazo ya moja kwa moja miongoni mwa vilabu vya ligi ya Uingereza kuanzia msimu ujao pamoja na tishio la kushushwa kutoka kwa ligi hiyo ndio sababu kuu ya vilabu kuwekeza kwa lengo la kusalia katika ligi hiyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pep Guardiola kushoto na Emanuel Pellegrini Kulia

Habari kubwa ya siku katika ligi hiyo hatahivyo ni ile ya uteuzi wa mkufunzi badala ya uhamisho.Manchester City ilitangaza kuwa Mkufunzi wa kilabu ya Bayern Munich Pep Guardiola atachakua mahala pake Manuel Pelergini mwishoni mwa msimu huu.

Mikataba mikubwa iliowekwa katika siku ya mwisho ya Uhamisho.

Siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho ni siku kuu katika soka ya Uingereza,lakini msimu huu huenda haukuwafurahisha waangalizi wengi.

Image caption Viilabu vilivyo chini ya jedwali

Mikataba iliofanyika yenye thamani ya pauni milioni 10,iliwasusha wachezaji wasio na umaarufu wowote miongoni mwa mashabiki wa ligi ya Uingereza, huku Stoke ikimsajili mchezaji wa kiungo cha kati Imbula,ikiwa ndio usajili mkubwa katika siku hiyo ya mwisho nayo Everton ikamuajiri mshambuliaji wa Senegal Niasse.

Watford iliwasajili wachezaji wawili kwa kitita kisichojulikana na kuwatoa kwa mkopo kwa kilabu ya Granada. Usajili wa kiungo wa kati wa kilabu ya Rennes Abdoulaye Doucoure na ule wa mshambuliaji Adalberto Penaranda imeripotiwa kuwa wa thamani ya pauni milioni 16 huku ukizifanya kilabu hizo kufanya matumizi ya juu kwa kitita cha pauni milioni 34.

Uhamisho mwengine mkubwa wa Uingereza katika siku ya mwisho ulitoka Middlesborough ambayo ilitumia pauni milioni 9 ili kumnunua mshambuliaji Jordan Rhodes kutoka kwa wapinzani wao Blackburn.Hakuna kilabu miongoni mwa timu nane bora katika ligi kuu ya Uingereza iliomsajili mchezaji yeyote.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Daniel Amartey

Licha ya matumizi hayo kupanda juu,vilabu hivyo havikufanya ununuzi wowote.Huku viongozi wa ligi hiyo kwa sasa Leicester ikimsajili Beki Daniel Amartey kutoka Copenhagen kwa pauni milioni 6 pamoja na winga wa Birmingham Demarai Gray kwa gharama ya pauni milioni 3.7, Arsenal ni timu ya pekee ya ligi ya Uingereza iliomsajili kiungo wa kati wa Basel Mohammed Elneny kwa pauni miloni 5.

Manchester City ilimsajili Anthony Caceres,lakini ikamtoa kwa mkopo kwa kilabu ya Melbourne City huku Tottenham na Manchester United zikikosa kumnunua mchezaji yeyote.

Gharama ya matumizi yaliofanywa na vilabu 6 vilivyopo chini ya ligi ya Uingereza ni pauni milioni 90 ikiwa ni nusu ya jumla yote ya matumizi ya ligi hiyo.Mwaka uliopita vilabu vilivyopo katika nafasi hizo zilitumia pauni milioni 20,ikiwa ni upungufu wa asilimia 20 kwa jumla.

Image caption Jonjo Shelvey

Mikataba miwili mikubwa kabla ya siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho ilifanywa na kilabu ya Newcastle kwa kitita cha pauni milioni 12 kwa kiungo wa kati wa Swansea Jonjo Shelvey na Winger wa Tottenham Andros Townsend wote wakiwa na wachezaji wa kimataifa wa Uingereza.

Bournemouth ilitumia jumla ya pauni milioni 16 kwa washambuliaji Lewis Grabban na Benik Afobe, huku Norwich ikimnunua Steven Naismith kwa pauni milioni 8.5.Huku timu nyingi zinazopigania kusalia katika ligi hiyo zikijaribu kuimarisha vikosi vyao, timu ya Aston Villa iliwaachilia wachezaji watano waondoke mwezi Januari na kukaa bila kusajili mchezaji yeyote.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mkufunzi Remi Garde

Mkufunzi wa Aston Villa Remi Garde ameripotiwa akibadili msimamo wake baada ya kusema mwezi uliopita kwamba wanahitaji wachezaji wapya iwapo wanahitaji kusalia juu.

Mchezaji wa West Brom Saido Berahino alitakikana na timu nyingi katika uhamisho wa pili kwa mfululizo, lakini alishindwa kuhamia kilabu yoyote.

Ombi la kilabu ya Tottenham la pauni milioni 22.5 kumununua mchezaji huyo wakati wa msimu wa joto lilikataliwa,na kumfanya Berahino kutishia kufanya mgomo,huku akikosa kuchezeshwa mara kwa mara tangu wakati huo.Newcastle iliwasilisha ombi la kitita cha pauni milioni 21 siku ya jumapili, lakini West Brom ikakataa kumuuza.

Image caption Alexi Texeira

Liverpool nayo ilikatwa tamaa baada ya jaribio la kumsajili mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk Alex Texeira mwenye umri wa miaka 26.Liverpool ilitoa kitita cha pauni milioni 24.5 kwa mchezaji huyo raia wa Brazil lakini haikuweza kufikia mahitaji ya kilabu hiyo ya pauni milioni 39.

Viongozi wa ligi kwa sasa Leicester walitoa ombi la pauni milioni 18.7 kwa mshambuliaji wa CSKA Moscow, Ahmed Musa mwenye umri wa miaka 23,lakini haikuweza kuafikia mahitaji ya kilabu hiyo ya pauni milioni 22.8 ili kumnunua.Pia walishindwa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Loic Remy kwa mkopo.

Hii ni kwa sababu the Blues walidhani kwamba mshambuliaji wa Colombia Radamel Falcao ataondoka Stamford Bridge kabla ya kukamilisha mkopo wake kutoka Monaco,lakini uhamisho wake kwa kilabu ya Atletico Madrid haikufanikiwa.