Neymar kutoa ushahidi wa uhamisho wake

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Neymar

Mchezaji wa Brazil Neymar anatarajiwa kutoa ushahidi katika mahakama moja ya Uhispania kuhusu madai ya ufisadi yanayozunguka uhamisho wake katika kilabu ya Barcelona.

Aliyekuwa rais wa kilabu hiyo pamoja na yule wa sasa wamekana kufanya makosa yoyote katika uhamisho huo siku ya jumatatu.

Barcelona inasema ililipa Yuro milioni 57 kwa ununuzi wa Neymar mwaka 2013,huku wazazi wake wakipokea Yuro milioni 40 na kilabu ya Brazili Santos ikipokea Yuro milioni 17.

Lakini uchunguzi unasema kuwa ada hiyo ilikuwa karibu Yuro milioni 83 na Barcelona ilificha kiasi kikubwa cha mkataba huo.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na kampuni ya uwekezaji ya DIS ambayo ilimiliki asilimia 40 ya haki za michezo za nyota huyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Barcelona

DIS inadai kwamba iliathiriwa kifedha na uhamisho huo ilipopokea Yuro milioni 6.8 za Yuro milioni 17 zilizolipwa kilabu ya Santos na kwamba ilinyimwa haki yake.

Rais wa kilabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu na mtangulizi wake Sandro Rosell walifikishwa mahakamani mjini Madrid siku ya Jumatatu,wakisisitiza kuwa hawakukiuka sheria zozote.

Babaake Neymar na mamaake pia walitarajiwa kufika katika mahakama hiyo ya kitaifa mjini Madrid.